Apps kumi zinazotumika sana Tanzania | Android

Kuna apps nyingi sana kwenye playstore, na hizi ndizo zinazo pakuliwa sana na watumiaji wa Android Tanzania.
Uwe na Tecno, Samsung, LG, Itel n.k lazima uwe na apps mbili au zaidi kati ya hizi.
Ili ufurahi na simu yako hakikisha walau una apps 8 kati ya hizi 10, ukiwa nazo zote ni bora zaidi.
Kuna apps nyingi sana kwenye playstore, na hizi ndizo zinazo pakuliwa sana na watumiaji wa Android Tanzania.
Uwe na Tecno, Samsung, LG, Itel n.k lazima uwe na apps mbili au zaidi kati ya hizi.
Ili ufurahi na simu yako hakikisha walau una apps 8 kati ya hizi 10, ukiwa nazo zote ni bora zaidi.
10. Likee
-Hii ni app inayojumuisha video nyingi fupi fupi. Inafanana sana na Snapchat lakini Likee ni rahisi kutumia na ina muonekano rafiki zaidi kwa watumiaji.
Kwenye Playstore Likee imepakuliwa zaidi ya mara milioni 100 duniani kote. Watu milioni 3 na zaidi wametoa maoni yao kuhusu Likee na imepewa nyota 4½ kati ya nyota 5.
Hii app ina mb 50
9. Beauty Plus - Easy Photo Editor & Selfie Camera
  - Kwa wapenzi wa picha na kujipendezesha hii ndo app yao.
  - Hii app inatumia camera ya simu kupiga picha nzuri. Licha ya kupiga picha nzuri tu pia unaweza ku-edit picha na kuifanya iwe katika hali ya kupendeza zaidi.
App hii ina mb 57 na imepakuliwa zaidi ya mara milioni 100 dunia nzima. Watu zaidi ya milioni 4 wametoa maoni yao kuhusu Beuty Plus - Easy Photo Editor & Selfie Camera na wameipa nyota 4½ kati ya 5.
8. Gboard - Google Keyboard
- Katika baadhi ya simu app hii inawekwa toka kiwandani. Lakini wengi wetu tunaotumia simu kutoka china app hii mpaka tuipakue.
Gboard ni app inayotumika kuandikia. Unaweza kuifanya ikawa rahisi kwa namna unavyotaka. Ina emojis ambazo ukiipakua tu zinakuja moja kwa moja. Pia ina picha zinazotembea/gif. Pia unaweza kubadilisha muonekano wa picha  nyuma ya maandishi ikawa ni picha yako binafsi. Hii ni app ya Google kwahio ni bora sana hasa kwa watumiaji wa Android.
  - App hii ina mb 24 na imepakuliwa zaidi ya mara milioni 500. Watu zaidi ya milioni 3 wametoa maoni yao na wameipa nyota 4.4 kati ya 5.
 
Download Gboard
7.  VLC
- VLC kama ilivyo kwenye computer na kwenye simu ina nguvu ile ile. Hii ni app kwa ajili ya kuangalizia video ulizo-download.
  - App hii inapanga videos zinazofanana kwa pamoja. Pia unaweza kuongeza mwanga na sauti za video kwa bila kuhama kwenye video.
  - App hii ina mb 25 na imepakuliwa zaidi ya mara milioni 100 duniani kote.
  - Watu zaidi ya milioni 1 wametoa maoni yao kuhusu VLC na wameipa nyota 4.4 kati 5.
6.  Chrome
  - Google chrome ni app inayotumika kuingilia mtandaoni/browser.
  - Chrome inamuonekano mzuri na ina uwezo kuonyesha tovuti kwenye simu kama zilivyo kwenye kompyuta.
  - Tofauti na app nyingine za kuingilia mtandaoni, Chrome ina uwezo wa kuangalia dokumenti, kuangalia videos na kusikiliza sauti.
  - Chrome imepakuliwa zaidi ya mara bilioni tano duniani kote na ina mb 30.
  - Watu zaidi ya milioni 16 wametoa maoni yao kuhusu Chrome na wameipa nyota 4.5 kati ya 5.
5.  Messenger
  - App hii ni kwa ajili ya meseji za facebook. Kuna pacha wa App hii ambayo ni Messenger Lite.
  - Ubora wa hii app ni kwamba inaweza kutumika pia kama njia ya kutumika kutuma meseji za kawaida bila intaneti.
  - Ukiwa na Facebook ni bora uwe na Messenger pia ili ufanikiwe kutuma meseji.
  - Messenger imepakuliwa zaidi ya mara bilioni 1duniani kote na ina mb 38.
  - Watu zaidi ya milioni 68 wametoa maoni yao kuhusu Messenger na wameipa nyota 4.2 kati ya 5.
4. Instagram
  - Instagram au Insta ni app maarufu sana duniani. Mtumiaji wa insta anaweka picha, videos na kutazama picha na videos za watu/account anazo-follow.
  - Insta sasa ina sehemu mpya ianyoonesha videos zenye muda mrefu. Sehemu hiyo inaitwa IGTV.
  - Instagram imepakuliwa zaidi ya mara bilioni moja duniani kote na ina mb 31.
  - Watu milioni 87 wametoa maoni yao kuhusu Instagram na wameipa nyota 4.5 kati ya 5.
3. YouTube
YouTube app ndio inayoongoza kwa kuwa na videos duniani. Kuanzia nyimbo za wasanii, muvi, series, michezo n. K
Ukiwa na app ya YouTube pia unaweza kutengeneza Chanel yako binafsi na kuweka videos zako binafsi.
  - Zaidi ya watu bilioni tano wamepakua app ya YouTube duniani kote na ina mb 35.
  - zaidi ya watu milioni 54 wametoa maoni yao kuhusu YouTube app na wameipa nyota 4.4 kati ya 5.
2. Facebook
  - zaidi ya asilimia 98 watanzania wanatumia Facebook. Facebook ni muhimu kwa habari, kuwasiliana na jamaa, kuweka kumbukumbu na mambo mengi zaidi.
  - unaweza kutumia Facebook kukutana na watu wapya( kupata wachumba/wenza) pia kutafuta kazi n.k
  -  kama hauna Facebook app kuna Facebook Lite ambayo ina mb chache.
  - Watu zaidi ya bilioni moja duniani kote wameipakua Facebook na mb 41.
  - Watu zaidi ya milioni 90 wametoa maoni yao kuhusu Facebook na wameipa nyota 4.2 kati ya 5.
1. WhatsApp
  - Hii ndio app iliyo ndani ya kila smartphone Tanzania ( ukiacha wachache ambao wameamua kukimbia michango kwenye magrupu ). Wasapu / Wasap/ Whatsapp ni app ya mawasiliano.
  - Unaweza kutuma meseji, sauti, dokumenti, videos na miziki.
  - Ukiiweka Whatsapp kwenye simu yako hautojutia.
  - WhatsApp imepakuliwa na watu zaidi ya bilioni moja duniani kote na mb 34.
  - Watu zaidi ya milioni 95 wametoa maoni yao kuhusu Whatsapp na wameipa nyota 4.4 kati ya 5.
Download WhatsApp
List hii itakua updated kila tarehe 15 ya kila mwezi.
Ukubwa wa App unategemea na aina ya simu.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kudownload Movies na Series mtandaoni kwa Simu | Android

Jinsi ya kudownload series za kikorea | Android

Jinsi ya kuinstall apps ulizo-download nje ya Playstore | Android